David Beckham anapenda kutizama mchezo wa nyota hawa sita
Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid ametaja
majina nyota sita Ulaya anaopenda kuwatizama.
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England aliulizwa wachezaji gani wanamsisimua zaidi kwa mchezo wao ambapo aliwataja Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney na nyota wengine wanne.
"Mbali na wanaofahamika na wengi-ningeweza kusema Leo na Cristiano -nadhani Morata ni mchezaji anayesisimua" aliiambia Sport360.
"Verratti kwa PSG. Nimecheza nae, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa.
"Na bila shaka Neymar.
"Kuna wachezaji wengi wakubwa mbali na hapa.
"Upande wa England ,ninaweza kusema Wazza.
"Wayne Rooney anacheza vizuri kwa United na wamekua na mwanzo mzuri wa msimu."
Beckham alicheza mechi 374 kwa United kabla hajahamia Real Madrid mwaka 2003 ambako alicheza mechi 159.
David Beckham anapenda kutizama mchezo wa nyota hawa sita
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 01, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment