Propellerads

Cheki Kimwaga alivyokua 'kichinjio' cha Simba kwa Stand United




Mshambuliaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka klabu
ya Azam FC leo ameing’arisha Simba baada ya kuifungia goli pekee kwenye mchezo wa leo dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.



Kimwaga aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Said Ndemla alifunga goli hilo muda mfupi baada ya kuingia baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Stand kisha kubaki yeye na nyavu na kufunga goli hilo kwa urahisi.

Licha ya Simba kutawala mchezo kwa asilimia nyingi lakini bado walishindwa kupachika mipira kambani kutokana na nafasi nyingi walizotengeneza.

Stand United walicheza vizuri na kuwazuia washambuliaji wa Simba kitu ambacho kiliongeza presha kubwa kwa wekundu hao ambao walilala kwa bao 2-0 kwenye mchezo uliopita dhidi ya watani zao Yanga.

Kimwaga aliisumbua safu ya ulinzi ya Stand United tofauti na mchezaji Boniphace Maganga ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati wa Simba kutokana na kukosekana kwa Hamisi Kiiza na nahodha wa timu hiyo Mussa Mgosi ambao wamekuwa wakianzishwa kama washambuliaji kwenye kikosi hicho.

Kocha mkuu wa Stand Leiwig leo hakuwepo kwenye benchi la timu yake kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi mbili.
Cheki Kimwaga alivyokua 'kichinjio' cha Simba kwa Stand United Cheki Kimwaga alivyokua 'kichinjio' cha Simba kwa Stand United Reviewed by Steve on Wednesday, September 30, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.