Picha:Taswira jinsi Yanga walivyowanyonga Mtibwa Sugar leo
Timu ya Yanga imeendeleza ubabe kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya
leo kuitandika timu ya Mtibwa Sugar kwa goli 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa dakika ya 58 kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Malimi Busungu baada ya baada ya beki wa Mtibwa Andrew Vicent kumrudishia mpira golikipa wake Said Mohamed lakini Busungu akainasa pasi hiyo na kupachika bao.
Wakati mpira ukitarajiwa kumalizika wakati wowote, Yanga waliandika goli la pili lililofungwa na mshambuliaji Donald Ngoma kufuatia golikipa Said Mohamed kutema shuti ambalo lilipigwa na Simon Msuva.
Picha:Taswira jinsi Yanga walivyowanyonga Mtibwa Sugar leo
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:

















No comments:
Post a Comment