Kuhusu penati waliyopata jana Man United, Van Gaal ana haya ya kusema
Meneja wa Man United, Louis van Gaal amedai kua mwamuzi
alikua sahihi kabisa kuwapatia penati kwenye mechi ya jana ya klabu bingwa ambapo waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolfsburg.
Ingawa kocha huyo Mholanzi amesema kua kushika mpira kwa Daniel Caligiuri kulistahili penati hiyo, lakini amekiri timu yake ilipata bahati ya kupata penati.
"Ilikua ngumu sana kwa sababu walifunga mapema sana. Lakini tulicheza vizuri ,tulitengeneza nafasi nyingi . Hatukuzimalizia, na nadhani penati ilikua ya bahati" aliiambia BT Sport.
"Bila shaka ni penati, lakini kuna baadhi ya waamuzi wasingepuliza kipenga pale. Tulitengeneza nafasi nyingi zaidi, Rooney na Depay wangeweza kufunga na kumaliza mchezo.
Juan Mata alisawazisha goli la Caligiuri kwa penati kipindi cha kwanza kabla ya Chris Smalling hajatupia bao la pili na la ushindi kwa Man United kipindi cha pili.
Kuhusu penati waliyopata jana Man United, Van Gaal ana haya ya kusema
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 01, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment