Wachezaji wa Chelsea wanajiandaa kwa hili kutoka kwa Jose Mourinho

Wachezaji katika kikosi cha Chelsea wanajiandaa na kuondoka kwa kocha
wao Jose Mourinho hapo baadaye, hii ni kwa mujibu wa ripoti.
Ripoti zimedai kua kocha huyo Mreno anaweza kutimliwa endapo kikosi chake kitakosa ushindi dhidi ya Liverpool kwenye mechi ijayo ya Premier League.
Hata hivyo, wachezaji wengi kwenye kikosi cha Chelsea wanaamini kua kocha huyo mwenye miaka 52 ataondoka, haijalishi matokeo yatakuwaje kwenye mechi ya jumapili na Liverpool.
Pamoja na Blues kua na kiwango kibovu msimu huu, inasemekana hakuna matatizo yoyote dhidi ya Mourinho kwenye chumba cha kubadilishia nguo , ingawa wachezaji wana wasi wasi kuhusu tabia ya kocha wao katika ligi kwa mujibu wa The Mirror.
Mourinho amekua na matukio ambayo yanahusisha kupigwa faini baada ya kumkosoa mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Southampton na lile la kumshambulia kwa maneno daktari wa timu, Eva Carneiro bila kusahau tukio jingine lililopita dhidi ya West Ham ambapo alikwaruzana na mwamuzi na kujikuta akitolewa kwenye benchi la ufundi.
Matukio yote haya ukijumlisha na kiwango kibovu , wachezaji wa Chelsea wanaamini kuondoka kwa kocha huyo katika wiki zijazo.
Wachezaji wa Chelsea wanajiandaa kwa hili kutoka kwa Jose Mourinho
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment