Hizi ni pongezi za Antony Martial kutoka kwa Wayne Rooney
mshambuliaji anayekuja kwa kasi, Antony Martial kwa namna alivyoweza kuzoea haraka maisha ndani ya Old Traford.
Mchezaji huyo alitua United akitokea AS Monaco ya Ufaransa siku ya mwisho kabla ya kufungwa dirisha la usajili kwa dau la pauni mil 36.
Usajili wake ulizua maswali kutoka kwa wadau wengi, lakini ameweza kufunga magoli matano katika mechi 10 za Premier League msimu huu.
Rooney ambaye nae pia alijiunga na Red Devils akiwa kijana mdogo, amesema Mfaransa huyo anastahili sifa za kutosha kwa namna alivyoweza kuendana haraka na mpira wa Uingereza.
"Nadhani amestaajabisha sana, jinsi alivyokuja Man United na alivyoanza," Rooney aliiambia United Review "Tusisahau kua bado ni kijana mdogo pia. Kuja akiwa kijana na kuanza kama ilivyo sasa, anastahili sifa sana.
"Unaweza kuona ni jinsi gani alivyo mchezaji mzuri na atakua muhimu sana kwetu mpaka mwisho wa msimu. Inaelekea ndiye mchezaji aliye haraka zaidi katika timu yetu, kama sio kwenye ligi."
Hizi ni pongezi za Antony Martial kutoka kwa Wayne Rooney
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment