Mkwasa atangaza kikosi cha Stars, Busungu, Maguli ndani
kikosi cha timu ya taifa kilicho tayari kupambana na Algeria.
Stars itaivaa Algeria katika mechi mbili mfululizo kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018, ikianza kwa kupambana nayo Novemba 17 jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17, ugenini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo huo.
Kikosi kamili alichokitaja Mkwasa kina wachezaji wapya sita ambao Salim Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Malimi Busungu, Ramadhani Kessy na Elius Maguli na kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).
Mkwasa atangaza kikosi cha Stars, Busungu, Maguli ndani
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 27, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment