Propellerads

Kufungwa kwa Simba, hii ndio furaha yake Cannavaro wa Yanga


                                           
                                                     

Beki na nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannvaro amefunguka kuwa
anafurahi kuona Simba inavyoyumba kwa sasa na wao wakizidi kuwaacha katika kuwania ubingwa na anaomba waendelee kuyumba mpaka mwisho wa msimu.

Yanga kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 19 sawa na Azam walio nafasi ya pili. Lakini Wanajangwani hao wapo juu kwa tofauti ya mabao. Simba yenyewe ipo nafasi ya tano ikifungana na Stand United iliyo nafasi ya nne kwa pointi 15.

Mpaka sasa Simba imefungwa michezo miwili na kushinda mitano wakati mahasimu wao Yanga wamefanikiwa kusinda mechi sita na kusuluhu mmoja mpaka sasa.

“Hiyo haina tatizo, kama Simba inafungwa na kuporomoka ndiyo sawasawa maana tunazidi kuiacha na inakuwa afadhali kwetu, tunapunguza watu tunaofukuzana nao huku juu, ikiendelea kufanya vibaya mpaka mwisho wa msimu hiyo itakuwa na faida sana,” alisema Cannavaro.


Pamoja na hayo, taarifa zinaeleza zaidi kuwa Simba sasa kunawaka moto kuhusiana na matokeo hayo na imeelezwa uongozi umemkalia kooni kocha wao, Muingereza, Dylan Kerr na kwamba ajira yake ipo mashakani.
Kufungwa kwa Simba, hii ndio furaha yake Cannavaro wa Yanga Kufungwa kwa Simba, hii ndio furaha yake Cannavaro wa Yanga Reviewed by Steve on Wednesday, October 28, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.