Propellerads

Van Gaal ataja mchezaj wa Man United mwenye uwezo zaidi wa kumiliki mpira




Bosi wa Manchester United, Louis Van Gaal amefichua kua ni mchezaji gani
wa kikosi chake anayedhani kua ana uwezo zaidi wa kumiliki mpira.

Van Gaal alijikuta akisema hivyo pale alipoulizwa kwanini aliamua kumtoa Bastian Schweinsteiger  kwenye mechi ya klabu bingwa jumatano dhidi ya Wolfsburg ambapo walishinda 2-1.

"Alikua amechoka nadhani ndio ilikua sababu, kwa sababu alianza kupoteza mpira na Schwensteiger kawaida ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kwa hiyo kwa sababu hiyo nikambadilisha," aliiambia tovuti rasmi ya klabu.

Kiungo huyo Mjerumani alikua mchezaji bora wa saba usiku huo akiwa na accuracy 79% huku Juan Mata (97.7%) Wayne Rooney (86.1%) kwa mujibu wa WhoScored.com.

Hata hivyo pamoja na kucheza dakika 71 pekee, Schwensteiger aliongoza kwa kutoa pasi kwenye kikosi cha Van Gaal akitoa pasi 62 mbele ya Daley Blind aliyetoa pasi 59.

Mchezaji huyo mwenye miaka 31 amecheza mechi 12 mpaka sasa na Man United, akianza michezo nane na kucheza dakika zote 90 katika michezo mitatu pekee.
Van Gaal ataja mchezaj wa Man United mwenye uwezo zaidi wa kumiliki mpira Van Gaal ataja mchezaj wa Man United mwenye uwezo zaidi wa kumiliki mpira Reviewed by Steve on Friday, October 02, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.