Propellerads

Ferguson afafanua kua alimaanisha nini kwa wachezaji aliowaita 'World class'




Sir Alex Ferguson ametetea madai yake kua alikua na
wachezaji wanne pekee Manchester United ambao walikua ni 'World class'.

Fergie mwenye miaka 73 sasa alikua kama meneja Man United kwa muda wa miaka 27, alitoa mapendekezo katika kitabu chake kipya kiitwacho Leading.

Kitabu kinaeleza kua Eric Cantona, Ryan Giggs, Paul Scholes na Cristiano Ronaldo pekee ndio wanaweza kuzungumziwa kama wachezaji World class.

Lakini Ferguson amefafanua kua wachezaji aliowataja walifanya vitu vya tofauti sana kwake.

"Hiyo ni sehemu ambayo vyombo vya habari havijaipa chapisho sahihi, sababu sahihi ya kusema hivi" Ferguson aliiambia redio moja ya Marekani iitwayo SiriusXM FC.

"Kama ukiangalia kipindi hicho nilichokua Man United kwa miaka 27, nilikua na wachezaji wazuri, wengine majina makubwa. Sijasema hao wachezaji hawakua wakubwa, walikua wazuri.

"Lakini kwa maoni yangu, yalikua ni maoni ya vigezo, kwamba wachezaji baadhi walionesha tofauti , na ndivyo nilimaanisha.

"Eric Cantona, alipokuja klabuni mwaka 1993 alionesha tofauti. Paul Scholes na Ryan Giggs wamecheza miaka 20 Premier League, hiyo imeonesha tofauti kwetu.

"Na bila shaka uwezo wa Cristiano Ronaldo ,ni mchezaji world-class kama kila mtu anavyojua. Yeye na (Lionel) Messi, wachezaji wawili world-class.
Ferguson afafanua kua alimaanisha nini kwa wachezaji aliowaita 'World class' Ferguson afafanua kua alimaanisha nini kwa wachezaji aliowaita 'World class' Reviewed by Steve on Friday, October 02, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.