Van Gaal anakerwa na maswali ya Wayne Rooney
Bosi wa Manchester United, Louis van Gaal amewaka kuhusu
kukosolewa kwa Wayne Rooney ambapo amesema hatajibu tena maswali yanayomhusu nahodha wake huyo.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30, alikosa nafasi nyingi za wazi kwenye mechi ya jana nyumbani dhidi ya Man City ambapo walitoa sare ya 0-0, ambapo kocha huyo mdachi aliulizwa kuhusu kiwango cha nyota huyo.
"Ninaongea kila wiki kuhusu Rooney, kwanini?" Van Gaal aliwaambia waandishi "Andika, ni maoni yako. Siwezi kutoa majibu zaidi kuhusu Roone kwa sababu nimechoshwa na hii."
Rooney amefunga magoli mawili pekee katika mechi tisa msimu huu.
Van Gaal anakerwa na maswali ya Wayne Rooney
Reviewed by Steve
on
Monday, October 26, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment