Mourinho kuitimuliwa endapo tu ikiwa hivi
Jose Mourinho anaweza kutimuliwa kuifundisha Chelsea endapo
Liverpool wakishinda mechi Stamford Bridge jumamosi ijayo, hii ni kwa mujibu wa ripoti.
Mbio za Chelsea kutetea ubingwa wao wa Premier League zimeingia mashakani tena baada ya kupoteza kwa 2-1 mbele ya West Ham jumamosi ambapo ni mechi ya tano wakishindwa msimu huu.
Kocha huyo Mreno alitolewa benchini baada ya kitendo chake kwa mwamuzi kufuatia kutolewa kwa Nemanja Matic.
Hata hivyo, uongozi wa Chelsea umeonekana kutopendezwa na mwenendo wa kocha huyo, ambapo kwa mujibu wa The Mirror endapo akipoteza mechi ijayo dhidi ya Liverpool huo ndio utakua mwisho wake.
Uvumi uliopo ni kwamba mmiliki wa klabu Roman Abramovich anafikiria kumleta kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola kuchukua nafasi yake.
Kwa sasa matajiri hao wa London wako nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi, point 11 nyuma ya vinara Man City na Arsenal.
Mourinho kuitimuliwa endapo tu ikiwa hivi
Reviewed by Steve
on
Monday, October 26, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment