Van Gaal amuonya Memphis Depay

Bosi wa Man United, Louis Van Gaal amemuonya nyota wake
Memphis Depay kua ni lazima aendane na falsafa ya klabu hiyo vinginevyo ataishia kua kama kina Agel Di Maria au Radamel Falcao.
Di Maria na Falcao walikiua na wakati mgumu klabuni hapo kutokana na kushindwa kua katika viwango vyao hivyo kuishia kuondoka.
Memphis alitua United akitokea PSV Eindhoven kwa dau la pauni milioni 25 baada ya kung'ara na waholanzi hao.
Hata hivyo, winga huyo bado hajawa na mwanzo mzuri Premier League na alikua benchi kwenye mechi ambayo Man United wameshinda 3-0 kwa Everton.
"Wachezaji wengine wanashindwa kuendana na falsafa ya timu," Van Gaal aliwaambia waandishi.
"Huwezi kujua mapema. Lakini unaona.
"Kwa sababu unaona ubora mwingi kwa mchezaji,lakini Depay anatakiwa kuutumia ubora wake kwa timu.
"Hiyo ilitokea pia kwa Di Maria na Falcao- wote ni wachezaji wakubwa lakini unatakiwa kuendana na falsafa. Sio kwa Memphis tu, kwa kila mchezaji tuliemnunua."
Hata hivyo, Van Gaal bado ana imani kubwa na nyota huyo ambaye pia katika klabu bingwa msimu huu alionesha makali yake.
"Kwamba bado namuamini?, bila shaka," aliongeza
Van Gaal amuonya Memphis Depay
Reviewed by Steve
on
Monday, October 19, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment