Propellerads

Ifikapo wakati huu huenda Falcao akaitema Chelsea






Imeripotiwa kua Radamel Falcao ameamua kuchukua
uamuzi wa kuachana na Chelsea ifikapo mwezi Januari baada ya kujaribu kua katika kiwango chake bila mafanikio akitokea AS Monaco kwa mkopo.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29 amefunga goli moja pekee akiwa kama mshambuliaji chaguo la tatu nyuma ya Diego Costa na Loic Remmy hapo Stamford Bridge.

Hivyo, Mkolombia huyo anaangalia uwezekano wa kurejea Ligue 1 majira ya baridi kwa mujibu wa The Mirror.

Falcao, ambaye aliweza kufunga mabao manne pekee kipindi alipokua kwa mkopo Man United msimu uliopita, inasemekana pia huenda akatemwa hata timu ya taifa.

Kwa hiyo itabidi Chelsea na Monaco kuvunja makubaliano ya mkataba wao ili kumruhusu nyota huyo kuondoka.

Barca wameripotiwa kutaka kumsajili Falcao.




Ifikapo wakati huu huenda Falcao akaitema Chelsea Ifikapo wakati huu huenda Falcao akaitema Chelsea Reviewed by Steve on Monday, October 19, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.