Propellerads

Pamoja na matokeo mazuri, huu ndio wasiwasi wa Pluijm msimu huu

                        

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema
kazi bado ni ngumu pamoja na mwenendo mzuri wa kikosi chake.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema Ligi Kuu Bara ambayo wao ni mabingwa inaonekana itakuwa ngumu kwa muda wote.

“Ligi haiwezi kupungua ugumu, itakwenda hivi. Hata kama kuna timu zitajigawa kwa maana ya  ubora lakini haziwezi kuwa chache.
“Hata ukiwa na timu tano au sita katika ligi ambazo ni imara, maana yake ligi ni ngumu na inatakiwa kupambana mwanzo ahdi mwisho,” alisema Pluijm.
Yanga imecheza mechi sita, imetoka sare moja na sasa iko kileleni ikiwa na pointi 16, sawa na Azam FC.

Yanga na Azam FC ndiyo timu pekee ambazo hazijapoteza hata mechi moja.
Pamoja na matokeo mazuri, huu ndio wasiwasi wa Pluijm msimu huu Pamoja na matokeo mazuri, huu ndio wasiwasi wa Pluijm msimu huu Reviewed by Steve on Tuesday, October 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.