Propellerads

Dondoo za leo Arsenal vs Bayern Munich kutoka kwa Shaffih Dauda

            
Leo michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inaendelea
kwa mechi kadhaa za makundi kupigwa, mchezo ambao umeteka masikio na macho ya wapenda soka wengi duniani ni ule kati ya Arsenal dhidi ya Bayern Munich utakaopigwa kwenye dimba la Emirates.
Arsenal wanahitaji ushindi dhidi ya Bayern Munich ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu hatua ya makundi kwenda hatua ya mtoano. Wakati huo wanacheza na Bayern timu ambayo imecheza michezo 12 kwenye mashindano yote bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski yuko kwenye ubora wa hali ya juu katika kupachika mabao, lakini pia kwa upande wa Arsenal wanajivunia Alexis Sanchez ambaye pia yupo kwenye kiwango kiuri cha kutupia nyavuni.
Arsenal inakutana na Bayern ikiwa imepoteza michezo yake miwili ya UEFA Champions League dhidi ya Dinamo Zagreb na Olympiacos. Timu hizo zimekutana mara mbili mfululizo kwenye hatua ya 16 bora misimu ya 2012-13 and 2013-14 na mara zote Arsenal imekua ikiondolewa kwenye mashindano hayo.
Hizi hapa ni rekodi za Arsenal na Bayern Munich kwenye baadhi ya michezo ambayo wameshakutana.

Arsena vs Bayern records
Dondoo za leo Arsenal vs Bayern Munich kutoka kwa Shaffih Dauda Dondoo za leo Arsenal vs Bayern Munich kutoka kwa Shaffih Dauda Reviewed by Steve on Tuesday, October 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.