Van Gaal achanganywa na timu yake

Louis van Gaal amefunguka jinsi timu yake ilivyo na shida katika
swala la umaliziaji mipira baada ya kutolewa Capital Cup na Middlesbrough.
Red Devils walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzifumania nyavu mpaka mchezo ukaishia kwenye hatua ya matuta.
Van Gaal alishuhudia wachezaji wakubwa Wayne Rooney, Michael Carrick na Ashley Young wakikosa penati zao ambapo ilipelekea United kupoteza kwa penati 3-1.
"Tunatakiwa kutatua hili tatizo. Tuanze kumalizia nafasi," Van Gaal aliwaambia waandishi kama alivyonukuliwa na FourFourTwo.
"Tulikua na nafasi nyingi kuliko wapinzani wetu zaidi ya mechi ya Manchester City, lakini tulitakiwa kuzimalizia. sasa tumetengeneza nyingi zaidi ya dhidi ya Manchester City, lakini tulitakiwa kufunga.
"Tuna wachezaji wengi ambao wangeweza kufunga, lakini hawakuweza kufanya hivyo. Sio mchezaji mmoja pekee na hii inachanganya kidogo.
:Tumetoka League Cup, kwa hiyo tuko dissapointed. Tulikua karibu na inauma kupotezea hapa. Nimefurahishwa na kiwango cha baadhi ya wachezaji wangu, lakini wengine wameniangusha."
Man United hawana muda wa kutosha kujiuliza sana kuhusiana na matokeo haya kwani wanakabiliwa na mechi ya ligi jumapili hii dhidi ya Crystal Palace ugenini Selhurst Park.
Van Gaal achanganywa na timu yake
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment