Ushindi wa Simba mbele ya Coastal Union, kuna hili bado halijamridhisha kocha Kerr

Kocha wa Simba, Dylan Kerr amefurahia kikosi chake kupata ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, jana.
Ushindi huo katika Ligi Kuu Bara umemfanya Kerr aongeze pointi tatu, lakini hajaridhishwa na uchezaji wa kikosi chake.
Kerr raia wa England anaamini Simba ina kikosi bora, lakini hakikuonyesha kandanda safi na ushindi huo ulikuwa sawa na wa kubahatisha.
“Hatukucheza vizuri, hakukuwa na juhudi ya kutosha kuhakikisha ushindi unapatikana.
“Lazima tubadilike na kufanya kazi zaidi. Wanasimba wanategemea mambo mengi yabadilike kupitia kikosi hiki, mimi sinafurahia sana,” alisema.
Simba ilishindwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo huo na bahati ilipata bao la mapema kupitia Hamisi Kiiza.
Ushindi wa Simba mbele ya Coastal Union, kuna hili bado halijamridhisha kocha Kerr
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment