League Cup: Man United watolewa kwa penati,Liverpool, Man City zapeta kama kawa
Klabu ya Man United jana wameangukia pua baada ya kutolewa kwenye
michuano ya League Cup na Middlesbrough kwa jumla ya penati 3-1 baada ya sare ya 0-0 mpaka muda wa nyongeza, huku Wayne Rooney, Michael Carrick na Ashley Young wakikosa penati.
Liverpool mambo yalikua mazuri jana baada ya ushindi wa kwanza wa kocha Jurgen Klopp baada ya kuwatandika Bournemouth kwa 1-0 katika round ya nne League Cup. Goli la Red's lilifungwa na Nathaniel Clyne dakika ya 17'.
Mechi nyingine ilikua kati ya Man City na Crystal Palace katika dimba la Etihad, ambapo City wametoa kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5-1 kupitia Wilfried Bony 22', De Bruyne 44', Iheanacho 59', Toure 76' (penati), Garcia 80'.
League Cup
FT Liverpool 1-0 Bournemouth
FT Man City 5-1 Crystal Palace
FT Southampton 2-1 Aston Villa
FT Man Utd 0-0 Middlesbrough
Pens. (1-3)
League Cup: Man United watolewa kwa penati,Liverpool, Man City zapeta kama kawa
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 29, 2015
Rating:






No comments:
Post a Comment