Propellerads

Ripoti:Pedro ajutia kuhamia Chelsea


                         

Mshambuliaji wa Chelsea, Pedro ameripotiwa kujutia uhamisho wake
kutoka Barca kuja kwa kikosi hicho cha Mourinho.

Mchezaji huyo mwenye miaka 28, wiki iliyopita alifunguka kua ni ngumu kuuzoea mpira wa Uingereza na kwa mujibu wa The Express, Pedro amemwambia mchezaji mwenzie, Cesc Fabregas kua angejua asingeondoka kwa mabingwa wa Hispania.

Mhispania huyo wa kimataifa aliondoka Catalan ili apate timu ambayo ataweza kucheza zaidi na kikosi cha kwanza, lakini chapisho moja la kihispania Fichajes limedai kua Pedro anaweza kufikiria kurejea tena Camp Nou.

Pedro amecheza mechi nane kwenye michuano yote kwa Blues, akifunga goli moja.
Ripoti:Pedro ajutia kuhamia Chelsea Ripoti:Pedro ajutia kuhamia  Chelsea Reviewed by Steve on Thursday, October 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.