Propellerads

Santi Cazorla afichua kwanini amekua bora zaidi msimu huu

                     


Santi Cazorla amemsifia kocha wake wa Arsenal, Arsene Wenger kwa
kumhamishia kiungo wa kati na kumfanya kua mchezaji bora Arsenal.

Katika msimu uliopita akiwa na Arsenal, Cazorla aliweza kufunga magoli saba na kusaidia mengine 11 katika mechi zote alizocheza.

Msimu huu bado hajafunga, ila ana furaha zaidi kwa kua na jukumu la kiungo Gunners.

"Bosi amebadilisha nafasi yangu msimu uliopita na kunichezesha kati zaidi," aliiambia Arsenal.com.

"Ni nafasi ninayoipenda kiukweli, japo inamaanisha nipo mbali na eneo la upinzani kwa hiyo nina nafasi chache za kufunga. Najiweka katika kiwango kizuri na ninafurahia nafasi mpya."


Santi Cazorla afichua kwanini amekua bora zaidi msimu huu Santi Cazorla afichua kwanini amekua bora zaidi msimu huu Reviewed by Steve on Thursday, October 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.