Tetesi: Ikitokea Mourinho akaondoka, Chelsea wanamtaka kocha huyu

Meneja wa klabu ya Atletico Madrid ya Hispania,
Diego Simeone anaweza kua mrithi wa Jose Mourinho kama akiondoka Chelsea, hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza.
The Blues wamekua na mwanzo mbaya kabisa kwenye Premier League tangu Roman Abramovich aimiliki klabu hiyo miaka 12 iliyopita, na inaaminika kua hana furaha na hali ya sasa.
Kwa mujibu wa Daily Mirror, Chelsea wanamwangalia kwa karibu meneja wa Atletico, Diego Simeone kama mbadala wa Mourinho ikitokea akatimka.
Mabadiliko haya yataweza kuigharimu zaidi Stamford Bridge kwani Mourinho na Simeone tayari wamesaini mikataba mingine vilabuni mwao.
Diego Simeone mkataba wake mpya unamfunga Atletico Madrid mpaka mwaka 2020 ukiwa na gharama ya Euro mil 20 kama ikitokea ukivunjwa huku akipikea kiasi cha Euro mil 5 kwa mwaka.
Mourinho anahitaji suluhisho la haraka kuitoa Chelsea katika kiwango kibovu, vinginevyo The Blues wanaweza kutafuta mtu mwingine wa kusimamia benchi la ufundi-pamoja na kwamba hivi karibuni ilitoa tangazo la kuendelea kumuunga mkono meneja huyo.
Kikosi cha Mourinho tayari kipo nyuma kwa point 10 kwa vinara Man City huku wakiwa wamechuma point nane pekee katika michezo nane waliyocheza.
Tetesi: Ikitokea Mourinho akaondoka, Chelsea wanamtaka kocha huyu
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 14, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment