Kumbe Evra kuhama Man United hayakua maamuzi yake!!

Patrice Evra amefichua kua kuhama Manchester United
hayakua maamuzi yake.
Mchezaji huyo mwenye miaka 34 alijiunga na mabingwa wa Serie A Juventus mwaka 2014 baada ya kutumikia Old Trafford miaka nane.
Beki huyo wa kushoto alikua ni kipenzi cha mashabiki wengi na kapteni wa klabu ambaye ilikua ngumu kuziba pengo lake baada ya kuondoka.
Hata hivyo Mfaransa huyo amefichua kua hayakua maamuzi yake kuondoka klabuni hapo, ila alifanya kwa ajili ya familia yake.
"Lilikua ni chaguo lililofanywa na familia yangu,"Evra aliiambia Redio moja ya Ufaransa iitwayo RMC.
"Ni ngumu kuongelea kwa sasa, iliumiza moyo. Lakini nilifanya maamuzi kwa ajili ya familia yangu. Sitaki kuongelea zaidi.
"Manchester United hawakutaka niondoke, lakini kabla ya kumalizika msimu wa ligi niliwaambia nataka kuondoka.
"Lilikua ni chaguo zuri , lakini sikutaka toka moyoni."
Kumbe Evra kuhama Man United hayakua maamuzi yake!!
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 13, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment