Habari kutoka Arsenal: Wenger agusia swala la kustaafu, pia wanamfukuzia nyota anaewindwa na Chelsea

Arsene Wenger amedokeza kua ataacha kuifundisha
Arsenal ndani ya miaka miwili ijayo.
Mkataba wa sasa wa Wenger unafikia ukomo mwaka 2017 ambapo katika mkutano mkuu wa klabu wa kila mwaka amegusia anataka kuacha urithi kwa atakayemfatia.
"Ninataka kufanya ushujaa kabisa mpaka siku ya mwisho ya mkataba wangu ili kuleta mafanikio kwa hii klabu, na kuondoka huku nikiiacha ikiendelea kufanya vizuri," Wenger alisema kama alivyonukuliwa na The Mirror.
"Hii ni muhimu kwangu kwamba naiacha klabu ikiwa na hali ambayo mtu atakayekuja badala yangu atafanya vizuri."
Pia Wenger anawachukulia Chelsea kama washindani wakubwa .
The Blues wameanza vibaya msimu huu katika kutetea taji lao, huku wakiwa nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.
Lakini Wenger anawapa matumaini makubwa.
"Chelsea wana mazingira ya kujitengeneza. Ni tofauti kwa kila mtu wakati huu, hata Chelsea." Wenger alinukuliwa na Daily Star.
"Bila shaka ukiwa na timu nyingi juu ni kazi ngumu kuzikamata."
The Gunners wana mpango wa kumnasa Jesse Rodriguez.
Nyota huyo ambaye Chelsea pia wameonesha nia ya kumhitaji, lakini kwa mujibu wa Sport Arsenal nao wanataka saini yake.
Habari kutoka Arsenal: Wenger agusia swala la kustaafu, pia wanamfukuzia nyota anaewindwa na Chelsea
Reviewed by Steve
on
Friday, October 16, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment