Propellerads

Ferguson afafanua kwanini hawakumtaka Silva




                           
Kocha wa  zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amefafanua
kwa nini aliamua kuacha kumsainisha David Silva kabla ya Mhispania huyo kujiunga na mahasimu wao Manchester City.

Ferguson amefichua kua Red Devils walichunguza uwezo wa nyota huyo kipindi alipokua Valencia, lakini waligundua Silva hakua na uwezo wa defense( kujilinda).

"Tulimwangalia alipokua Valencia, Alikua ni namba 10 mzuri lakini hakua na uwezo wa kulinda," alisema Fergie kama alivyonukuliwa na AS.

"Kama mchezaji anataka kufanikiwa, anatakiwa kujituma na kutetea. Daima inaniwia ugumu sana kupata wachezaji kama hawa."

Silva alijiunga na City mwaka 2010 kwa dau la €28.75 million ambapo mpaka sasa ameichezea klabu hiyo mechi 232 huku akifunga magoli 40 na kusaidia mengine 85.




Ferguson afafanua kwanini hawakumtaka Silva Ferguson afafanua kwanini hawakumtaka Silva Reviewed by Steve on Friday, October 16, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.