Hii hapa mipango binafsi ya De Gea msimu huu

David De Gea anataka kua katika kiwango alichokua nacho
msimu uliopita Manchester United.
Mhispania huyo alichaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka jana Man United na tayari ameshaanza kampeni yake katika kiwango kizuri pamoja na kufungwa magoli matatu na Arsenal kwenye mechi yao ya Premier League.
De Gea hakufungwa goli lolote na kuokoa hatari zote kwenye mechi ambayo timu ya taifa ya Hispania ilishinda 1-0 mbele ya Ukraine usiku uliopita kufuzu Euro mwakani.
Kocha Vincele Del Bosque amempanga kipa huyo kama chaguo la kwanza kwa Hispania kwa sasa ambapo De Gea ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri ili kuendelea kua namba moja kwa nchi yake.
"Timu yote ilikua na mechi nzuri," De Gea aliiambia TVE kufuatia ushindi dhidi ya Ukraine.
"Tulijua kua tunaenda kwenye uwanja mgumu kupambana na timu ngumu inayotaka kushinda, kwa hiyo ulikua ni ushindi mzuri kwetu.
"Hua najitahidi kufanya ninaloweza na nilicheza vizuri. Ilikua ni muhimu kushinda, kwa hiyo nina furaha sana. Tulikua na bahati, lakini tunatakiwa kuendelea kucheza kama hivi.
"Najitahidi kucheza kiwango changu cha juu wakati wote na ninataka kumpa kocha kazi ngumu kuchagua namba moja wake kuelekea Euro.
"Ninataka kua katika kiwango nilichokua msimu uliopita, ambacho nadhani kilikua kikubwa. Ni vigumu kudumu, lakini nataka kuendelea kukua na kua bora."
Hii hapa mipango binafsi ya De Gea msimu huu
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 13, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment