Mbali na Man City, Aguero anataka kufanya kazi na kocha huyu

Nyota wa Man City, Sergio Aguero amefunguka kua siku moja
anapenda kufanya kazi chini ya kocha Pep Guardiola.
Kocha huyo mhispania kwa sasa anaifundisha Bayern Munich, lakini kuna tetesi kuhusiana na hatma yake klabuni hapo kwani mkataba wake unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu.
Wiki iliyopita huko Hispania kulikua na ripoti kua Guardiola amefanya makubaliano ya mdomo kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini kuifundisha City msimu ujao, na sasa Aguero ameongelea jinsi anavyomkubali kocha huyo mwenye mafanikio.
"Ningependa kufundishwa na yeye hapo baadae kwa sababu ni bonge la kocha, lakini leo nina furaha na Manuel Pellegrini." Aguero alisema kama alivyonukuliwa na The Mirror.
Mkataba wa sasa wa Pellegrini na Etihad utafika ukomo ifikapo majira ya joto 2017.
Mbali na Man City, Aguero anataka kufanya kazi na kocha huyu
Reviewed by Steve
on
Monday, October 12, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment