Propellerads

Wenger au Mourinho kumrithi kocha wa sasa wa PSG!!

Wenger, Arsenal, AFC, Mourinho, Chelsea, CFC, PSG, latest Chelsea news

ArseneWenger na Jose Mourinho wametajwa na vyombo vya
habari vya Ufaransa kua miongoni mwa wanaoweza kumrithi kocha Laurent Blanc kuifundisha Paris Saint-Germain.

Mabingwa hao wa Ligue 1 wamekua na mwanzo mzuri kutetea taji lao ambapo kwa sasa wapo katika usukani mwa ligi.

Lakini kwa mujibu wa ripoti, huku nafasi ya Blanc ikiwa bado ya kuridhisha tu, uongozi wa klabu tayari una mipango mingine msimu huu.

Goal wanadai kua Blanc anaweza kutimuliwa kutokana na kutofanya vyema michuano ya klabu bingwa.

Inadhaniwa kua bosi wa Chelsea, Jose Mourinho ni miongoni mwa wanaopewa kipaumbele zaidi kwenye nafasi hiyo.

Kocha huyo Mreno aliwahi kua na mazungumzo na klabu hiyo kabla hawajamchukua Blanc.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger pia yumo kwenye orodha ya makocha wanaotakiwa na PSG japo aliwahi kukataa ofa za mabingwa hao mara tatu huko nyuma , pia kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola naye yumo katika mipango hii.



Wenger au Mourinho kumrithi kocha wa sasa wa PSG!! Wenger au Mourinho kumrithi kocha wa sasa wa PSG!! Reviewed by Steve on Tuesday, October 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.