Mourinho kama kawaida yake, arusha zigo la lawama kwa wachezaji wake
Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake kufuatia kupoteza mchezo wa klabu bingwa Ulaya
dhidi ya Porto kwa 2-1.
Meneja huyo wa Chelsea alikasirika Porto walipopata ushindi wao pale Maicon alipofunga kwa kichwa mpira wa kona.
"Kwetu ni makosa ya kijinga" alisema Mourinho "Tuliangalia Porto wakirudia kona mara nyingi. Nadhani tulikua tayari kwa hilo. Lakini katika wakati ambao mchezo tuliutawala na tunajiandaa kubadili matokeo, iko wazi goli lilikua kama barafu kwa wachezaji.
"Kitu cha msingi katika mpira ni mpangilio wa ulinzi, mpira umesimama, unalinda nafasi au mtu au vyote. Tulikua na kosa jingine kama hilo (kutokea kwenye kona) pale walipopiga nguzo."
Mourinho hakuwaweka washambuliaji Radamel Falcao, Loic Remmy pia Oscar ambapo amesema ni sababu ya kimbinu na kwamba hajutii "Mbali na hayo makosa mawili, mchezo ulibalance." alisema.
Baada ya kupoteza mchezo huo wa jana, Chelsea wamejikuta wakitoka juu ya kundi na kuangukia nafasi ya tatu.
Mourinho kama kawaida yake, arusha zigo la lawama kwa wachezaji wake
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment