Ospina alivyowagharimu Arsenal ambapo Wenger ametoa madai haya
Hatma ya Arsenal kwenye klabu bingwa ulaya kwa sasa iko
katika hatihati kufuatia makosa ya mlinda mlango David Ospina.
Mkolombia huyo aliitwa golini badala ya Petr Cech na kocha Arsena Wenger ambapo alifanya makosa katika kona na ambapo Arsenal walijikuta wakipoteza mchezo wa pili mfululizo katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.
Baada ya mchezo huo Wenger amesema "Ni usiku mbaya kwangu kwa klabu bingwa? Hapana. Kukaa kwenye benchi na kupoteza fainali. Kuona makosa ya golikipa ni kitu cha kawaida.
Ospina amecheza michezo 23 na kuokoa mikwaju hatari 10 msimu uliopita, alikua na mchezo safi zaidi wiki iliyopita dhidi ya Tottenham.
"Hakuna golikipa asiyefanya makosa. Hiyo inaweza kutokea hata kwa Petr Cech.
"Siwezi kukaa hapa na kua nawaelezea watu juu ya kila maamuzi ninayoyafanya. Nawaacha watu wajaji. Lakini sio sababu hiyo tukapoteza mchezo,
"Ninafanya maamuzi na uchaguzi na nina wajibu. Ninajua vitu vingi ambavyo watu hawajui na ndio maana wanadharau ninapofanya maamuzi. Siwezi kufanya maamuzi ambayo yatafata mawazo ya kila mtu"
Kocha huyo wa Gunners akasema tena "Hii imetuacha sisi katika nafasi mbaya, lakini bado tumo. Tunatakiwa tushinde nyumbani dhidi ya Bayern, hatuwezi kuepuka hii."
Ospina alivyowagharimu Arsenal ambapo Wenger ametoa madai haya
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 30, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment