Propellerads

Hatimaye Rooney afunguka kuhusu kutaka kuhama mwaka 2013




Nahodha wa England na klabu ya Manchester United,
Wayne Rooney amefunguka kua kamwe hakuomba kuondoka Old Trafford mwaka 2013.

Miaka miwili iliyopita kabla ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mshambuliaji huyo alijikuta katika kizungumkuti na klabu yake ya Man United, na sasa mwenyewe ameweka wazi kwa kile ambacho watu walikua hawajui kuhusu uvumi wa yeye kuomba kuondoka.

"Nilienda kumuona (Ferguson) na nikasema tu 'kama hutanichezesha mimi ni bora nikaondoka'," Rooney ameeleza kupitia documentary ya BBC.

"Halafu ghafla, ilienea kwenye vyombo vyote vya habari kua nimeomba kuondoka. Sijui ni nini kilitokea, kwanini ilikua vile."

Rooney pia alizungumzia uhusiano na meneja wake huyo wa zamani ambapo amesema sasa wako vizuri zaidi ya miaka miwili iliyopita.

"Sio mimi tu niliyewahi kutofautiana na Alex Ferguson. Nadhani ni wachezaji wengi tu. Baadhi waliondoka. Baadhi walikaa."

Rooney ameisaidia klabu yake ya Manchester United kukaa kileleni mwa ligi baada ya ushindi dhidi ya Sunderland mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hatimaye Rooney afunguka kuhusu kutaka kuhama mwaka 2013 Hatimaye Rooney afunguka kuhusu kutaka kuhama mwaka 2013 Reviewed by Steve on Wednesday, September 30, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.