Propellerads

Manchester United wako tayari kuvunja mkataba na Valdes ila tu asijiunge na vilabu hivi



Manchester United wanadaiwa kua tayari kuvunja mkataba na mlinda mlango wao
Victor Valdes endapo tu atakubali kutimkia nje ya Premier League.

Kipa huyo mhispania ameonekana kususwa Old Trafford baada ya kukataa kucheza timu ya vijana msimu uliopita.

Msimu huu hakuruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza huku Van Gaal hakumpa nafasi yoyote hata kama David De Gea hakuwepo.

Na sasa kwa mujibu wa Daily Mail, United wako tayari kuvunja mkataba wake ambao ungeisha mwishoni mwa msimu huu napia kumlipa mishahara yake yote iliyobakia.

Lakini hawako tayari kumruhusu kujiunga na mahasimu wao wakiwemo Chelsea ambao wameonesha kuvutiwa nae.

Liverpool nao pia walihusishwa na Valdes kabla hajajiunga man United ambapo waliamua kumchukua Simon Mignolet.

Kwa sasa Chelsea wanahitaji kipa mwingine ambapo Thibaut Courtois yuko nje akisumbuliwa na majerahah huku Jose Mourinho akionekana kua na wasi wasi kutokana na kumtegemea Asmir Begovic pekee.




Manchester United wako tayari kuvunja mkataba na Valdes ila tu asijiunge na vilabu hivi Manchester United wako tayari kuvunja mkataba na Valdes ila tu asijiunge na vilabu hivi Reviewed by Steve on Tuesday, September 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.