Yanga vs Azam, cheki uchambuzi na mambo kedekede hapa
Leo unapigwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam
dhidi ya Yanga mchezo unaoashiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la ligi kuu Tanzania bara kwa msimu mpya wa 2015-20116. Mechi hiyo itachezwa kwnye uwanja wa Taifa kuanzia saa 10:00 jioni.
Mechi hiyo inazikutanisha timu ambazo zimekuwa na upinzani mkubwa kwa siku za hivi karibuni, Yanga ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita wakiwa wameinyang’anya Azam ubingwa huo iliokuwa ikiutetea kwa msimu huo. Azam wao ni mabingwa wa kombe la Kagame 2015 wakitwaa kombe hilo kwa kuifunga Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya matuta.
Mtanange wa leo unatarajiwa kuwa ni mgumu kutokana na maandalizi yaliyofanywa na kila timu, falsafa za makocha, ubora wa wachezaji na historia ya timu hizo kwenye kikombe hicho cha Ngao ya Jamii.
Yanga waliweka kambi yao jijini Mbeya ambapo walicheza mechi tatu na kufanikiwa kushinda zote wakati wapinzani wao walikuwa Zanzibar ambako nao walicheza mechi tatu za kirafiki na kushinda mechi zote. Hii pia inatoa sura ya ugumu wa mchezo wa leo.
Falsafa za makocha:
Kocha wa Azam, Stewart Hall: Tangu kurejea kwake Azam kumekuwa na utofauti mkubwa kwenye kikosi cha hicho ambapo kwa sasa wanacheza mpira wa kasi na kushambulia sana hasa kupitia pembeni kwa kuwatumia Shomari Kapombe na Michael Gadiel. Lakini eneo la ulinzi limeonekana kuimarika zaidi na hiyo ilidhihirika kwenye michuano ya Kagame ambapo Azam haikuruhusu goli hata moja tangu kuanza hadi kumalizika kwa michuano hiyo.
Ukuta wa Azam unatengenezwa na Wawa akishirikiana na Agrey Morris, wakati Mugiraneza, Domayo, Himid Mao wakitarajiwa kuongoza safu ya kiungo na John Bocco pamoja na Kipre Tchetche wao watakuwa wakicheza kama washambuliaji.
Mfumo wa Azam FC: 3-5-2
Kocha wa Yanga, Van Pluijm: Anapenda soka la pasi nyingi fupifupi na kushambulia muda wote, mashambulizi ya timu yanatengenezwa na viungo wa katikati na mara kadhaa viungo wa pembeni ambao kwa sasa wanaopewa nafasi kucheza nafasi ya viungo wa pembeni ni wachezaji wapya Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke.
Amis Tambwe na Dolnald Ngoma ni washambuliaji ambao maranyingi wanapewa nafasi ya kucheza pamoja wakati safu ya ulinzi ya Yanga ikiongozwa na mabeki wawili wakongwe, Kelvin Yondani na Nadir Horoub ‘Cannavaro’ wakati Niyonzima akipewa majukumu ya kuongoza safu ya viungo wa kati.
Mfumo wa Yanga SC: 4-4-2
Wachezaji wakuchungwa kwenye mchezo wa leo:
Yanga: Wachezaji wakuchungwa kwa upande wa Yanga ni Donald Ngoma, Amis Tambwe, Deus Kaseke, Mwashiuya na Busungu. Wachezaji hao wote walionesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Kagame japo walitolewa na Azam kwenye hatua ya robo fainali.
Azam: John Bocco amekuwa akifunga sana kwenye mechi za Simba na Yanga, hivyo Yanga wanapaswa kuwanayemakini muda wate. Kipre Tchetche, Gadiel Michael ni wachezaji wengine wanaohitaji uangalizi wa hali ya juu.
Wachezaji wapya ambao wanaweza kupewa nafasi kwenye mechi ya leo.
Yanga: Kuna wachezaji wapya wawili wa Yanga ambao wamecheza mechi za kirafiki lakini mashabiki wanahamu kubwa kuwaona leo kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, kiungo aliyenunuliwa kutoka FC Platinum ya Zimbabwe Thaban Kamusoko na mlinzi wa Togo Vincent Bossou ambao leo wanaweza kupewa nafasi kwenye kikosi cha Van Pluijm.
Azam: Ramadhani Singano ‘Messi’ ni mchezaji wa zamani wa Simba kila mtu anajua uwezo wake awapo uwanjani, mchezo wa leo Messi anaweza akapewa nafasi ya kuonesha uwezo wake akicheza kwa mara ya kwanza mechi ya mashindano akiwa na klabu ya Azam. Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Azam wameshapata nafasi ya kucheza isipokuwa kwa mshamuliaji Alan Wanga ambaye yupo nyumbani kwao kwenye msiba wa mama yake.
Historia ya Azam na Yanga kwenye kombe la Ngao ya Jamii:
Azam haijawahi kutwaa Ngao ya Jamii, mara zote ilizopata nafasi ya kucheza kuwania taji hilo imepoteza mechi zote na kutoka mikono miupu. Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ilikuwa ni msimu wa 2014-2015, Yanga ilishinda kwa goli 3-0 na kutwaa taji hilo.
Matokeo ya mechi tano zilizopita kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC
Julai 29,2015: Azam 0-0 Yanga ( penati: Azam 5-3 Yanga)
Mei 6, 2015: Yanga 1-2 Azam
Desemba 28, 2014: Azam 2-2 Yanga
Machi 19, 2014: Yanga 1-1 Azam
Septemba 22, 2013: Azam 3-2 Yanga
Yanga vs Azam, cheki uchambuzi na mambo kedekede hapa
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 22, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment