Propellerads

Hii ndio sababu iliyomfanya Van Gaal leo kumuanzisha Schwensteiger badala ya Carrick



Kocha Louis van Gaal ameeleza kwanini ameamua kumuanzisha
Bastian Schwensteiger katika kikosi cha kwanza badala ya Michael Carrick mchezo wa leo.

Schwensteiger alicheza michezo mitatu iliyopita akitokea benchi lakini leo dhidi ya Newcastle amecheza nafasi ya Carrick.

Van Gaal ameiambia BT Sport " Ninahitaji kumjenga (Schwensteiger), kama unataka kumchezesha  mchezaji zaidi ya dakika 45 inabidi umuanzishe"

"Kila mtu anasema ni bingwa wa dunia na ameshinda vitu vingi lakini yeye kama mchezaji anatakiwa kuthibitisha hilo

"Kufanya hivyo kwa Manchester sio rahisi lakini namuamini sana.

"Nataka nimweke sawa Carrick kwa mechi zingine. Msimu uliopita alikua na majeraha kwa hiyo nataka kuzuia hiyo" alimaliza.
Hii ndio sababu iliyomfanya Van Gaal leo kumuanzisha Schwensteiger badala ya Carrick Hii ndio sababu iliyomfanya Van Gaal leo kumuanzisha Schwensteiger badala ya Carrick Reviewed by Steve on Saturday, August 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.