Propellerads

Usajili Ulaya: Dau la £60m la Chelsea kwa Pogba lakataliwa, Man United wanamtaka Neymar, Benzema kupima afya jumatatu




Dau la puni milioni 60 la Chelsea kwa Pogba
limekataliwa na klabu ya Juventus.

Matajiri hao wa London walitoa dau la pesa na pia kumtumia mchezaji Juan Cuadrado kama sehemu yadili ili kunasa saini ya nyota huyo.

Hata hivyo Juve wamekataa ofa hiyo ambapo inadaiwa Mourinho anajipanga tena kurudi kivingine.



Manchester United nao wanadaiwa kufanya mawasiliano na klabu ya Barcelona kuangalia uwezekano wa kumnasa Neymar, tayari mtendaji wa Red devils, Edwoord Park amedaiwa kumwekea dau ambalo bado halijajulikana.

Gazeti la The Sun linasema kua Man United wana mpango wa kumpata nyota huyo mwenye miaka 23 baada ya kushindwa kumpata Pedro.

Chanzo kutoka Barca kililiambia gazeti hilo "United ni miongoni mwa klabu kubwa ulimwenguni kwa hiyo ni sawa kabisa kumfukuzia mchezaji ambaye ana nafasi kubwa ya kua nyota zaidi pia yulimwenguni"



Kwingineko, klabu ya Arsenal wanajiandaa kukamilisha usajili wa Benzema kabla ya mechi yao na Liverpool wiki ijayo.

Mwandishi wa habari za soka wa Italia, Emanuele Giulianelli amedai kua tayari Arsenal wamemtumia ndege Benzema ili aje kupima afya Jumatatu.

"Inaaminika Arsenal wamekodi ndege binafsi ili kumleta Benzema jumapili jioni" Giulianelli aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

"Atachukua vipimo vya afya mapema mchana na itathibitishwa kabla ya mechi, atakaa katika hoteli ya nyota tano katikati ya London"









Usajili Ulaya: Dau la £60m la Chelsea kwa Pogba lakataliwa, Man United wanamtaka Neymar, Benzema kupima afya jumatatu Usajili Ulaya: Dau la £60m la Chelsea kwa Pogba lakataliwa, Man United wanamtaka Neymar, Benzema kupima afya jumatatu Reviewed by Steve on Saturday, August 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.