Tetesi: Van Gaal awaambia watu wa karibu anamtaka Bale
Imeripotiwa kua kocha Louis Van Gaal amewaambia watu
wake wa karibu kua anamhitaji nyota Gareth Bale klabuni Manchester United.
United walihusishwa sana na nyota huyo hata kabla hajajiunga na Real Madrid mwaka 2013 na pia mwanzoni mwa msimu wa 2014/15 na ripoti za sasa zinadai bado Red Devils bado wana nia na Bale.
Gazeti la Daily Maily linadai kua kocha huyo amewaambia rafiki zake kua anataka kumleta Bale kutoka Los Blancos na anaamini mchezaji huyo atawapa nguvu kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu.
Bale amepata kuichezea Real Madrid meci 92 mpaka sasa, akifunga magoli 39 na kutoa usaidizi mara 31.
Tetesi: Van Gaal awaambia watu wa karibu anamtaka Bale
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 22, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment