Jose Mourinho ajilaumu mwenyewe na wachezaji wake kwa kuanza vibaya msimu huu.
Kesho Chelsea wataumana na West Brom huku wakitarajia ushindi kwa mara ya kwanza wakiwa na nyota wapya, Pedro na Baba Rahman.
Akiongelea hali ya sasa Mourinho amesema haya kama alivyonukuliwa na Express
"Sina furaha na fomu yangu ya sasa, kwa sababu nimezoea kupata matokeo mazuri kuliko nayopata sasa" akaongeza tena "Sina furaha na kiwango cha Branislav Ivanovic, Gary Cahill,John Terry, Cesar Azpilicueta, Cesc Fabregas, Nemanja Matic lakini kitu cha kwanza sina furaha na kiwango changu"
"Kwa hiyo tulichokua tukifanya wiki hii ni kua makini zaidi mazoezini, kuangalia video na kujituma zaidi.
"Kwa sasa naenda gym kila siku kujiweka sawa, labda nahitaji kufanya zaidi nikiwa kazini, kwa hiyo nahitaji kua fit"
Mourinho anatarajiwa kukipanga tena kikosi chake kwa kumrudisha John Terry katika nafasi kama kawaida, pia kuisha kwa adhabu ya kipa Thibaut Courtois, hata hivyo inadaiwa daktari Eva Carneiro na mwenzie Jon Fearn wa upande wa afya bado hawataonekana benchini.
Jose Mourinho ajilaumu mwenyewe na wachezaji wake kwa kuanza vibaya msimu huu.
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 22, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment