Propellerads

Unaambiwa Lukaku ndie anamshauri John Stones 'atose' dili la Chelsea!!



Inadaiwa kua beki John Stones, anashauriwa kwa kiasi kikubwa na
mchezaji mwenzie Everton, Romelu Lukaku kua asiondoke baada ya kuhusishwa na kutengewa dau kubwa na Chelsea.

Kwa sasa Chelsea wako katika mpango wa ofa nyingine baada ile ya mwisho ya Pauni mil 30 kukataliwa.

Lukaku, ambaye aliondoka Chelsea mwaka jana baada ya kushindwa kuonesha makali yake, anaamini kua Stones anakua na nafasi kubwa zaidi ya kuchaaguliwa kwenye kikosi cha Euro 2016.

"Ki ukweli John yupo katika hali nzuri katika klabu ambayo wanamwamini sana" Lukaku alisema kama alivyonukuliwa na Mirror.

"Anacheza huku pia akijifunza mengi kutoka kwa Phil Jagielka. Amekua hapa kwa miaka miwili lakini huu ndio wakati wa yeye kuonesha kua ni mchezaji bora.

"Yupo hapa sehemu nzuri. Anahitaji kufanya anachotakiwa. Bado ana Euro inakuja, kwanini aondoke!!

Mkataba wa sasa wa Stones na Everton unaisha mwaka 2019.
Unaambiwa Lukaku ndie anamshauri John Stones 'atose' dili la Chelsea!! Unaambiwa Lukaku ndie anamshauri John Stones 'atose' dili la Chelsea!! Reviewed by Steve on Saturday, August 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.