Kocha Louis van Gaal aongelea dili lililokwama la Pedro, pia amtetea Ed Woodward
LOUIS VAN GAAL amesema hakuna mpasuko wowote uliotokea
kati yake na mtendaji wa timu hiyo Ed Woodward baada ya kushindwa kumsajili Pedro kutoka Barcelona.
Kocha huyo amedai kua ulikua ni mpango wake kuachana na mchezaji huyo ingawa hajaeleza sababu juu ya hilo.
Pedro alijiunga na Chelsea kwa kusthukiza wiki hii kwa dau la £21.3million japokua alikua akifukuziwa na Man United kwa muda mrefu.
Baada ya yote yaliyotokea, van Gaal hapendi kuongelea nini klitokea katika dili hilo, lakini alikua tayari kuzungumzia kile kinachoelezwa kutofautiana na Woodward ambaye alikasirikiwa na mashabiki wengi baada ya kumkosa Pedro, kocha van Gaal amesema hakuna tofauti yoyote walionayo.
"Nina imani kua unataka kunitenganisha mimi na Woodward" aliiambia Express "Lakini hapana, namuamini sana.
"Nadhani wao(mashabiki) hawana haja ya kua na shaka na Woodward, kwa sababu kwa miaka mingi amekua hapa na amejidhihirisha kua mtu sahihi.
Kuhusu Pedro, Van Gaal ameongea kwa umakini kidogo kwamba hajawahi kusema anataka kumsajili, ila tu kwamba alisema anafaa kua mchezaji wa Man United.
"Siwezi kujibu kuhusu haya maswali (kuhusu Pedro), unajua nini kama nilivyosema kua kila tunachofanya ni mchakato.
"Katika huo mchakato tunafanya maamuzi nadhani kama tungemtaka Pedro kulikua hamna tatizo lolote" Alimaliza kocha huyo mdachi
Pia baada ya kukanusha swala hilo la Pedro, van Gaal pia amekanusha taarifa zingine kwamba wanataka kumsajili Sadio Mane kutoka Southampton.
Kocha Louis van Gaal aongelea dili lililokwama la Pedro, pia amtetea Ed Woodward
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment