Propellerads

Arsene Wenger afunguka kuhusu usajili wa Benzema, ameongea maneno haya





Kocha Arsenal Wenger ameongea kuhusu usajili wa
Benzema, hii inafuatia kutoeleweka kwa swala hili huku likiwaacha mashabiki wengi wa Arsenal wakiwa na wasi wasi mwingi kama kweli dili hilo litakamilika.

Tayari Manchester United na Tottenham nao wameonesha nia ya kumnasa nyota huyo,

Katika majira haya ya joto, Arsenal wamekua wakihusishwa sana kutaka kumnasa Benzema, lakini swala hilo limekua likikwama kwani Real Madrid wamekua wakisita kumuuza, Wenger sasa ametoa kauli juu ya ishu hii na kusema kua mara nyingi hua ni swala gumu kwa makocha wengi kuimarisha safu ya ushambuliaji.

"Natarajia kumsainisha, kama kwa kila ambavyo mtu angependa kufanya, lakini pia bado hatuko karibu" alisema kama alivyonukuliwa na Express

"Nimemsikiliza kila mmoja, lakini kazi yangu ni kufanya maamuzi- hata kama nikimuuliza kila mtu. Kama ningesikiliza kila mtu tusingewasajili Patrick Vieira, Nicolas Anelka na Thierry Henry.

"Ni ngumu kwa sababu kuna pesa nyingi katika mpira na vilabu vyenye vyanzo vingi.

"Lakini hata hivyo kuna uhaba wa wachezaji namba 9 ulimwenguni, inathibitisha niliyoyasema , kwamba siku hizi kuna tofauti ya uwezo wa pesa na upatikanaji wa wachezaji viwango vya juu.

"Ni rahisi, kama unataka kununua inabidi ukaongee na mmiliki na kama hataki huwezi kununua.

"Sikatai kununua kama kuna mabadiliko yatapatikana kwa timu, lakini kama swala ni kununua mchezaji kufurahisha watu, siko tayari"

Hata hivyo Wenger aliwapa moyo mashabiki wa Arsenal kua anatarajia kumnasa Benzema muda wowote kabla ya kufungwa dirisha la usajili.



Arsene Wenger afunguka kuhusu usajili wa Benzema, ameongea maneno haya Arsene Wenger afunguka kuhusu usajili wa Benzema, ameongea maneno haya Reviewed by Steve on Friday, August 21, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.