Iniesta: Kamwe sitaweza kucheza EPL
Mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amefunguka kuhusiana na
kama ana mpango wa kuhamia ligi ya Uingereza baada ya nyota mwenzie Pedro kutimkia Chelsea.
Kapteni huyo wa Barca amesema kua kamwe hajawahi kushawishika kuachana na Barca na kwenda vilabu vya England na kwa sasa anaangalia tu mkataba wake Nou Camp.
"Sijawahi kufikiria hivyo" aliiambia El PaĆs.
"Nina furaha sana hapa na bado nina miaka mitatu katika mkataba wangu, natumaini nitaimaliza.
"Kwangu hakuna sehemu zaidi ya Barca.
"Na kama ukifikiria kitu kama hicho, huoni lolote"
Barca kwa sasa wamemruhusu Pedro ambaye ameeleka EPL, huku pia wachezaji wengine kina Yaya Toure, Cesc Fabregas, Deco na Alexis Sanchez waliondoka Blaugrana na kujiunga na vilabu vya EPL.
Iniesta amepata kucheza michezo 545 kwa Barca, akiifungia magoli 52 na kutoa usaidizi katika mashambulizi 52.
Iniesta: Kamwe sitaweza kucheza EPL
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment