Propellerads

Wenger nae azungumza kuhusu swala la daktari wa Chelsea na Mourinho




Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemtetea daktari wa
Chelsea, Eva Carneiro na kusema kua sheria za ligi ziko wazi  kua ni mwamuzi pekee ndiye anaweza kukataa kuingia kwa daktari uwanjani.

Caneiro alikwaruzana na Mourinho jumamosi iliyopita baada ya yeye na daktari mwingine kuingia uwanjani kumtibu Hazard kisha kumtoa kitendo ambacho Mourinho alichukia.

Kufuatia taarifa za sasa Mourinho kumtoa kwenye jopo la timu daktari huyo, Kocha Wenger ambaye ni hasimu mkubwa wa Mourinho, amesema ni kitendo kinachoonesha kutokua na umoja na itaweza kupelekea matatizo kambini.

"Inaweza kua tatizo ndani ya klabu" alisema Wenger kama alivyonukuliwa na Daily Mail  "Ni ngumu sana kama hamko pamoja. Kuaminiana na umoja ni umoja ni nguvu klabuni.

"Hii stori ya Chelsea sijaifatilia na sina chochote juu ya linaloendelea.
"Cha pili, sheria ziko wazi, kama refa akitoa ishara kwa madaktari kuingia, wanaweza kuingia.

"Baada ya haya yote sijui chochote, lakini sheria ziko wazi" alimaliza Wenger.
Wenger nae azungumza kuhusu swala la daktari wa Chelsea na Mourinho Wenger nae azungumza kuhusu swala la daktari wa Chelsea na Mourinho Reviewed by Steve on Friday, August 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.