Propellerads

Kuhusu hatma ya Ivo Mapunda, hii ndio kauli ya Rais wa Simba




Hatma ya Elius Maguri na Ivo Mapunda bado haijajulikana ndani ya
klabu ya Simba huku kila mchezaji akiwa na mazingira tofauti ya ama kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo au kutokuwepo kabisa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara 2015-2016.

Rais wa Simba SC Evans Aveva ameweka wazi kuwa hatma ya Elius Maguri iko mikononi mwa kamati ya usajili ya klabu hiyo kufuatia kocha wa klabu hiyo Dylan Kerr kumuengua katika kikosi chake katika mchezo wa Simba Day dhidi ya SC Villa.

Kuhusiana na mlindamlango Ivo Mapunda Aveva amesema klabu yake inasubiri pande hizo mbili  kukutana na kutiliana saini.

“Elius Maguri Jina lake halikuwepo kwa vigezo ambavyo mwalimu anavijua na sisi kama wanasimba na ‘stake holders’ wa mpira siku zote mmekuwa mkipigia kelele viongozi hasa wa vilabu vya Simba na Yanga tumekuwa tukiingilia majukumu ya walimu, sisi tukaona tuheshimu hilo pamoja na kwamba Maguri tulimsajili kwa matumaini makubwa”, amesema Evans Aveva

“Lakini mwalimu alipokuja akaona uwezo wa Maguri ni mdogo kwa hiyo katika ile mechi ya Villa Elius Maguri asishiriki, kinachofuata baada ya hapo ni maongezi pamoja na viongozi wa Simba kujua hatma yake.

Aveva pia ameweka wazi juu ya hatma ya golikipa Ivo Mapunda akisema kuwa, mazungumzo na Ivo yameshafanyika imebaki kutiliana saini kati ya pande hizo mbili.

“Ivo Mapunda ataendelea kuwa mchezaji wa Simba Sports Club katika kipindi kinachokuja”.

“Mazungumzo yalifikia hitimisho na wakakubaliana Ivo atakuja kusaini mkataba na klabu yetu ya Simba, mpaka hivi ninavyo zungumza ni kwamba ni bahati usajili umesogezwa mbele, kwa hiyo bado tuna muda lakini mpaka hapa ninavyozungumza Ivo bado hajaonekana kuja kusaini mkataba Simba hivyo jukumu hili limerudishwa tena katika kamati husika na Ivo bado yupo Dar tutatoa majibu”.
Kuhusu hatma ya Ivo Mapunda, hii ndio kauli ya Rais wa Simba Kuhusu hatma ya Ivo Mapunda, hii ndio kauli ya Rais wa Simba Reviewed by Steve on Friday, August 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.