Propellerads

Wenger : Liverpool watammkumbuka sana Raheem Sterling



Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kua Liverpool watakumbuka
sana mchango wa Raheem Sterling pamoja na kumsaji Roberto Firmino.

Liverpool walimuuza nyota huyo kwa Manchester City kwa dau la pauni mil 49 baada ya yeye kukataa kuongeza mkataba mpya klabuni hapo.

Hata hivyo klabu ilinunua wachezaji wengine, Firmino ambaye alitua kwa gharama za pauni mil 29 na Benteke pauni mil 32, pamoja na yote Wenger anaamini bado Liverpool watakumbuka uwepo wa Sterling ambapo aliziambia ripoti

"Binafsi namtazama Raheem Sterling. Hili tutaliona kwa muda mrefu. Sidhani kama Sterling alikua analeta visa. Ni katika kipindi cha usajili hayo yote yakatokea.

"Kipindi cha msimu alikua kimya-hakuongea chochote, sidhani kama aliongea sana. Ni mchezaji mwenye ubora, wamemnunua Firmino tutaona atakachofanya.

"Lakini ngoja tukumbuke miaka miwili iliyopita wakiwa na Suarez, Sterling na Sturridge walifunga zaidi ya magoli mia, kufunga magoli zaidi ya mia katika Premier League unahitaji ubora na Sterling alikua miongoni"

Arsenal na Liverpool wanaumana baadae leo katika mchezo wa Premier League.


Wenger : Liverpool watammkumbuka sana Raheem Sterling Wenger : Liverpool watammkumbuka sana Raheem Sterling Reviewed by Steve on Monday, August 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.