Fabregas amsifia Pedro mechi ya jana, adai ameongeza nguvu mpya
Cesc Fabregas amedai kua nyota mpya wa Chelsea ameongeza nguvu mpya
baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya West Brom jana.
Pedro ambaye alisaini Chelsea wiki hii kwa dau la 21.4 mil ameonesha makali yake kwa kuifungia Chelsea kwenye mechi ya jana ambayo ilikua ya kwanza kwake ambapo walishinda 3-2 dhidi ya West Brom.
Pia Pedro alitoa usaidizi kwa shambulizi la Diego Costa ambapo liliipa timu ushindi wake wa kwanza, Fabregas amemmwagiua sifa kibao nyota huyo
"Alikua vizuri sana, nilijua kabisa angefanya makubwa kwenye hii timu kwani kiuhalisia ni kitu ambacho hatukua nacho kabla.
Kwa sasa Chelsea wako katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kufuatia ushindi wa jana.
Fabregas amsifia Pedro mechi ya jana, adai ameongeza nguvu mpya
Reviewed by Steve
on
Monday, August 24, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment