Stars watua salama huko Uturuki
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili nchini Uturuki tayari kwa
kambi ya wiki moja kujiandaa kuivaa Nigeria.
Stars imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ataturk katika jiji la Istanbul nchini.
Baada ya kuwasili Istanbul ilianza safari hadi kwenye mji wa Kartepe ulio juu ya milima kabisa ambako wataweka kambi yao katika Hoteli kubwa ya kitali ya The Green Park.
Kumbuka Stars imesafiri kwa saa saba hadi Istanbul kupitia ndege ya Turkish ambayo iliondoka Dar es Salaam saa 9:45 alfajiri na kuwasili saa 4:45 asubuhi.
Taifa Stars chini ya Kocha Boniface Mkwasa, msaidizi wake, Hemed Morocco, Kocha wa Makipa, Manyika Peter pamoja na mshauri wa ufundi, Abdallah Kibadeni inatarajia kuanza mazoezi ya kwanza leo Saa 1 usiku.
Hoteli hiyo imezungukwa na viwanja vya kisasa kwa ajili ya maandalizi ya timu ambazo zimekuwa zikiweka kambi hapa.
Stars watua salama huko Uturuki
Reviewed by Steve
on
Monday, August 24, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment