Propellerads

Haya mengine kuhusu ishu ya Man United na Neymar



Ripoti mpya zinadai kua Neymar atasaini mkataba
mwingine wa pesa nyingi klabuni Barcelona na kuachana na uvumi wa Man United

Nyota huyo kwa sasa nae amekua akihusishwa sana na Man United huku The Guardian wakisema kua vyanzo vinadai Neymar anaweza kufikiria kuhamia Red Devils.

Hata hivyo mchambuzi mmoja wa La ligaGuillem Balague  ameibuka na kudai kua Neymar anatarajia kuongeza mkataba mwingine na wakali wa Catalan.

Mchambuzi huyo ame tweet "Neymar atasaini upya mkataba wake na Barcelona. Lakini kabla hajasaini stori nyingi zitatokea. Ni mchezo wa kizamani"

Neymar will renew his contract with Barcelona. But before he signs it, more stories will come out to put pressure to FCB. It is an old game

Iko wazi kua Neymar atataka kuongeza mkataba ambao utalingana na nyota wengine kama Messi na Suarez.

Kwa sasa Neymar anavuta kiasi cha £150,000 kwa wiki, huku Messi  £313,000 na Suarez  £200,000.
Haya mengine kuhusu ishu ya Man United na Neymar Haya mengine kuhusu ishu ya Man United na Neymar Reviewed by Steve on Monday, August 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.