Propellerads

Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha £50m



Kwa mujibu wa ripoti, nyota wa Real Madrid, Karim Benzema
anaweza kujiunga na Arsenal kama wakiweka dau.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akihusishwa na The Gunners ambao hata hivyo bado hawajaonekana kua na dau rasmi la kueleweka.

Hata hivyo chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Daily Star kua sasa ni kazi  ya Arsenal  kupigania saini ya nyota huyo kwa dau kubwa ambapo Real Madrid wameripotiwa kumthaminisha kwa kiasi kisichopungua pauni mil 50.

Iko wazi kua Arsenal wanaweza kupata ushindani mkubwa wa kumpata nyota huyo kutoka kwa Manchester United ambao nao walionesha nia ya kupata saini.

Benzema alikua nje wakati Real Madrid wakitoa sare na Sporting Gijon jumapili hii.
Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha £50m Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha  £50m Reviewed by Steve on Monday, August 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.