Wakala wa Neymar aeleza haya kuhusu Manchester United
Wakala wa nyota wa Barcelona Neymar amefunguka kua
Man United wanataka kumsajili mchezaji huyo na sasa wako katika mazungumzo.
Kumekuwapo na ripoti katika siku za hivi karibuni ambazo zinadai Man United wako katika mpango wa kumnasa nyota huyo mbrazil, na sasa wakala Pini Zahavi ameeleza kua kuna mazungumzo yanaendelea kwa mchezaji wake ambaye amemsifia kua ni bora zaidi duniani.
Akiliambia gazeti la The Sun amesema "Ni kawaida kwa klabu kubwa kama Manchester United kutaka kupata huduma ya mchezaji kama Neymar ambaye ni bora zaidi duniani.
"Itashangaza sana kama Man United wataachana na mpango kama huu, lakini kwa sasa wanafanya mambo"
Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 akitokea Santos.
Wakala wa Neymar aeleza haya kuhusu Manchester United
Reviewed by Steve
on
Monday, August 24, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment