Tambo za msenegali wa Simba, aahidi balaa
Mshambuliaji Papa Niang ametamba kwamba
atafuzu majaribio Simba bila ya hofu.
Niang ametua nchini kwa ajili ya kufanya majaribio na leo ataichezea Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati inaivaa Mwadui FC katika mechi ya kirafiki.
Niang amesema ana uhakika wa kufanya vizuri licha ya kwamba hakuwa na mazoezi ya kutosha.
"Kweli nilipumzika muda kidogo, lakini ninaamini uwezo wangu. Kwa mazoezi ya siku chache na mechi moja nitakayocheza, hakuna kitakachonizuia.
"Kuzungumza kuhusu mwenyewe si jambo jema, huenda itakuwa vizuri watu wakaniona nikiwa kazini,"alijitapa.
Msenegali huyo inaelezwa ni mdogo wa Papa Niang, mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal, Mamadou Niang.
Tambo za msenegali wa Simba, aahidi balaa
Reviewed by Steve
on
Monday, August 24, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment